FM Manyara
FM Manyara
2 December 2025, 8:36 pm

Madiwani kutoka kata za halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara wameapishwa rasmi leo kuanza kutekeleza majukumu yao pamoja na kufanyika uchaguzi wa kumchangua mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa Baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Babati.
Na Mzidalfa Zaid
Akitangaza matokeo hayo, Katibu tawala wilaya ya Babati Thobias Abwao amesema Yona Wao amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la madiwani kwa kwa kura zote 12 za wapiga kura na Salome Masasi ameshinda nafasi ya makamu mwenyekiti kwa kupata kura zote 12 za ndio.

Akizungumza kwa niaba ya ofisi ya mkoa wa Manyara, Afisa elimu ya watu wazima Ibrahim Mbogo , amewataka viongozi hao kutenda haki na kusimamia sheria pamoja na kusimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato.
Mwenyekiti wa Baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Babati Yona Wao amesema atafaata miongozo bila kumuonea mtu, ambapo amewaomba madiwani kumpa ushirikiano.

Nae makamu mwenyekiti wa Baraza hilo Salome Masasi , amemshukuru Mungu kwa kuchaguliwa na kusema kuwa atamshauri mwenyekiti katika kuhakikisha kazi zinafanyika vizuri.

Aidha, Mbunge wa jimbo la Babati mjini Mmmanuel Khambay amesema atashirikiana na viongozi hao huku akiwataka viongozi hao wasiwe chanzo cha migogoro badala yake wawe mstari wa mbele kushirikiana katika kuleta maendeleo ya wananchi.
