FM Manyara
FM Manyara
28 November 2025, 2:02 pm

Wakulima mkoani Manyara wametakiwa kulima kilimo cha kisasa kwa kutumia mbegu na viuatilifu bora pamoja na kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa kilimo katika maeneo yao.
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo Umetolewa na mwakilishi wa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati Grace Lambau wakati akiongea katika semina ya kilimo ambayo imeandaliwa na kampuni ya AgroGlobe Limited kwa kushirikiana na kampuni ya Fide mamba Agrovert kwa lengo la kuwaelimisha wakulima kuhusu kilimo bora .
Akizungumzia lengo la mafunzo hayo afisa mauzo wa kampuni ya Agroglobe limited kanda ya Pwani Alex King amesema wamewakutanisha wakulima hao kwa lengo la kuwapa elimu namna ya kuandaa kilimo bora.
Nae Meneja wa fide Mamba Agrovert Manka John, amesema mkulima anapaswa kutumia pembejeo bora ili apate mazao mengi na kuwa na uhakika wa kilimo chake.

Aidha,baadhi ya wakulima ambao wameshiriki Semina hiyo wamezishukuru kampuni hizo kwa kuwa wamefaham namna ya kuandaa kilimo cha kisasa ambapo wakulima hao wamepata nafasi ya kusajiliwa namba za ruzuku pamoja na kupimiwa udongo.
