FM Manyara
FM Manyara
27 November 2025, 4:31 pm

Mtandao wa jinsia tanzania (TGNP) imetoa mafunzo kwa kamati za viongozi ngazi ya vijiji na kata
Na Marino Kawishe
Mtandao wa jinsia tanzania (TGNP) umeendesha mafunzo yakuwajengea uwezo viongozi warakibishi waliopo kwenye kamati za mpango wa taifa wakutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto MTAKUWWA kutoka vituo vya taarifa na maarifa wilayani Mbulu na halmashauri ya wilaya ya Babati Mkoani Manyara.
Akizungumza na fm manyara radio mkufunzi wa warsha hiyo kutoka mtandao wa jinsia tanzania (TGNP) Deogratias Temba amesema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo wawakilishi hao ambao wataenda kuelimisha jamii na kuendeleza mapambano ya ukatili unafanyika kwenye maeneo yao.
Kwa upande wake mwakilishi wa washiriki wa warsha hiyo kutoka kata ya mamire Malik Kimaro amesema kumekuwa na mafanikio makubwa kwenye eneo la mamire na kukiri ukatili unaendelea kupungua kwa sababu ya mafunzo wanayopata mara kwa mara.
Warsha hiyo ya siku Tatu kuhusu mpango wa taifa wakutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na Watoto (MTAKUWWA) imeangazia pia masuala ya ustawi wa jamii na ukatili wa kijinsia na jinsi ya kukabiliana na kesi za ukatili pale zinapowasilishwa kwenye kamati za MTAKUWWA.
