FM Manyara

Dkt. Florence akagua majengo ya afya hospital ya mkoa Manyara

26 November 2025, 9:12 pm

picha ya Naibu waziri wa afya Dokta Florence George akisikiliza taarifa ya ujenzi wa majengo hayo

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Florence George amekagua ujenzi wa jengo ya damu salama, jengo la wagonjwa mahututi na jengo la wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.

Na Mzidalfa Zaid

Akizungumza baada ya ukaguzi wa majengo hayo, George ametoa maelekezo kuwa ujenzi wa majengo hayo ukamilike haraka na yaanze kufanya kazi kwakuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa wakati.

sauti ya Naibu waziri wa afya Dokta Florence George

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Manyara katibu tawala mkoa wa Manyara Mariam Muhaj amesema watatekeleza maagizo hayo na kukamilisha majengo hayo kwa wakati.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa majengo hayo  Kaim Mganga Mfawidhi hospital ya rufaa ya mkoa wa Manyara Yesige Mutajwaa, amesema ujenzi wa majengo hayo uko hatua za mwisho kukamilika .

sauti ya  Kaim Mganga Mfawidhi hospital ya rufaa ya mkoa wa Manyara Yesige Mutajwaa
picha ya  Kaim Mganga Mfawidhi hospital ya rufaa ya mkoa wa Manyara Yesige Mutajwaa

Aidha, mbunge wa jimbo la Babati mjini Emmanuel Kambay, ameishukuru serikali kwa kutenga bajeti hiyo kujenga majengo hayo ambapongeza wizara ya afya kwa kufatilia miradi hiyo.

sauti ya mbunge wa jimbo la Babati mjini Emmanuel Kambay
picha ya mbunge wa jimbo la Babati mjini Emmanuel Kambay