FM Manyara
FM Manyara
26 November 2025, 12:52 pm

Shirika la Umeme Tanzania Tanesco mkoa wa Manyara limeanza zoezi la kubadilisha Mita za umeme kwa kuondoa mita za zamani na kufunga mita janja (Smart Meters ) mita ambazo zitawezesha wateja pindi wanaponunua umeme kuingia moja kwa moja .
Na Mzidalfa Zaid
Afisa uhusiano wa Tanesco mkoa wa Manyara Samwel Mandar ameyasema hayo wakati akiongea na Fm Manyara, amesema zoezi hilo litafanyika nyumba kwa nyumba na zoezi hilo limeanzia wilayani Babati.
Aidha,amesema katika zoezi hilo salio la unit zinazobakia kwenye mita ya awali zitahamishiwa kwenye mita mpya inayowekwa na hakutakuwa na malipo yoyote katika uboreshaji huo.