FM Manyara
FM Manyara
26 November 2025, 12:24 pm

Kuelekea siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, wakulima wadogo Mkoa wa Manyara wametakiwa kujitokeza katika Madawati ya kisheria ili kupeleka changamoto za ukatili wanazo kutananazo.
Na Emmy Peter
Hayo yamesemwa leo na Mhandisi Agrey Mahole ambae amemuwakilisha mkuu wa wilya ya Babati katika ofisi za chama cha wakulima wadogo MVIWATA zilizopo wilayani Babati Mkoani Manyara Amesema wakulima wadogo wamekuwa wakipata changamoto hizo ya ukatili huo katika Maeneo hayo
Aidha Mratibu wa Mviwata Malkiadi Maega kutoka Tawi la Manyara Amesema wamefanya Mkutano na wananchama wa chama hicho kuelekea katika maadhimisho hayo kupinga siku 16 za ukatili wa kijinsi Ambapo amesema ukatili unaomgusa Mkulima Mdogo Ni tofauti na ukatili wa Mjini kwakuwa Inachangia kumkandamiza Mwanamkeee kiuchumi.
Kwa upande wao wanachama wa chama hicho wamemshukuru mkuu wa wilaya ya Babati kwa kuendea kuunga mkono juhudi za wanawake kiuchumi na kupeleka elimu vijijini na katika mabaraza la wazee ili kukemea ukatili huo.