FM Manyara
FM Manyara
19 November 2025, 12:17 pm

Wanafunzi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu mkoani Manyara wametakiwa kuacha kujiingiza katika makundi yasiyofaa ya kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya kwakua itachangia kushuka kwa elimu na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Na Mzidalfa Zaid
Akizungumza na Fm Manyara, afisa ustawi wa jamii kutoka Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kanda ya kaskazini Sara Ndaba amesema wanaendelea kutoa elimu katika vyuo vya kati na vyuo vikuu ndani ya mkoa wa Manyara katika kupambana na matumizi ya dawa za kulevya.
Ndaba amesema lengo la kufikisha elimu hiyo vyuoni ni kuwafahamisha madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ambapo amesema kuna baadhi ya wananafunzi wamejiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya na kushindwa kufikia malengo yao.

Kwa upande wake afisa elimu jamii kutoka Mamalaka ya kudhbiti na kupambana na dawa za kulevya kanda ya kaskazini Shaban Miraji, amesema mtu anapo jihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya anaweza kufanya vitendo visivyofaa na kujishushia utu wake ikiwemo uporaji au ugomvi.

Afisa TAKUKURU mkoa wa Manyara Mwinyi Hamisi amesema TAKUKURU wana utaratibu wa kutoa elimu kwa wanafunzi kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuoni ili waweze kuwasaidia kutoa taarifa pamoja na elimu dhidi ya rushwa na matumizi ya dawa za kulevya.
