FM Manyara
FM Manyara
15 November 2025, 11:44 am

Mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda amewataka wananchi wilayani Babati mkoani Manyara kutunza vyanzo vya maji ikiwemo kutofanya shughuli zao karibu na vyanzo hivyo.
Na Mzidalfa Zaid
Kaganda amesema hayo baada ya kukagua miradi ya maji ukiwemo mradi wa Darakuta na mradi wa chanzo cha maji Mrara, ambapo amewataka wananchi kuendelea kutunza vyanzo hivyo ikiwemo kutokata miti hovyo.
Amesema mradi wa chanzo cha maji Darakuta utanufaisha wananchi zaidi ya elfu30 na mradi wa chanzo cha maji Mrara utanufaisha wananchi zaidi ya elfu 20.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Babati(BAWASA) Iddi Msuya, amesema kata ya Nkaiti ni miongoni mwa kata ambayo itanufaika na mradi wa Darakuta.
Nao baadhi ya wananchi wa wilaya ya Babati ambao wanatarajia kunufaika na mradi huo, wamesema kutokana na changamoto ya maji waliyonayo, miradi hiyo itasaidia kutatua changamoto hiyo ya maji.