FM Manyara
FM Manyara
13 November 2025, 11:00 am

Mkuu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara Emmanuela Kaganda, amezindua kampeini ya nishati safi na kuhamasiha matumizi ya majiko salama kwa mazingira katika wilaya hiyo.
Na Mzidalfa Zaid
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaganda amesema kampeini hii itasaidia kutokomeza nishati chafu,kwani serikali imetenga fedha nyingi kwa kuandaa nishati safi ili kuwasaidia wananchi wa vijijini katika shughuli zao.
Kwa upande wake mhandisi wa miradi REA Ramadhani Mganga, amesema Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan, ametenga jumla ya shilingi bilioni 9 kuhakikisha kila mwananchi anatumia nishati safi na mkoa wa Manyara umepatiwa majiko zaidi ya 7000.
Mwakilishi wa kampuni ya LS SOLUTION LIMITED amesema majiko hayo yanatumia kuni kidogo hivyo yatasadia kupunguza gharama kubwa za matumizi ya kupikia.
Aidha baadhi ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Babati, ambao wamejitokeza kununua majiko hayo ya bei nafuu, wameishukuru serikali kwa kugharamia asilimia 80 ya bei ya majiko hayo .
