FM Manyara
FM Manyara
27 October 2025, 9:43 pm

Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania Mkoa wa Manyara imekutana kwa pamoja na kuliombea Taifa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu ili uchaguzi huo ufanyike kwa amani na utulivu bila kukumbwa na vitendo vya kuvunja amani.
Na
Akizungumzia lengo la kukutana kwa viongozi hao , Katibu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania Mkoa wa Manyara, Askofu Josia Sumaye amesema uchaguzi mkuu upo kikatiba hivyo wameamua kwa pamoja kufanya maombi na dua ili watanzania wapige kura na kumchagua kiongozi wanaemtaka kwa amani na utulivu .
Kwa upande wake, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania Juma Mkola, amewahimiza viongozi wa dini kuwaelimisha waumini wao kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura, akisisitiza kuwa Serikali imeweka mipango madhubuti ya kuimarisha ulinzi na usalama katika siku ya uchaguzi.
Aidha, viongozi wa dini kutoka madhehebu tofauti walipata nafasi ya kuomba na kuliombea taifa kuelekea uchaguzi mkuu.