FM Manyara
FM Manyara
21 October 2025, 5:30 pm

Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Babati mjini Simon Mumbee ametoa elimu ya upigaji kura kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika october 29 mwaka huu, ambapo amewataka wananchi kufika kwenye vituo vya kupigia kura kuanzia saa moja kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni.
Na Mzidalfa Zaid
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Babati Mumbee amesema jumla ya vituo 206 vinatarajia kutumika katika zoezi la upigia kura katika halmashauri ya mji wa Babati.
Aidha, amesema kwa wananchi ambao wamepoteza kadi za kupigia kura na waliandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ataruhusiwa kupiga kura endapo atafika katika kituo alichopangiwa akiwa na leseni ya udereva au pasi ya kusafiria au kitambulisho cha nida na majina ya kitambulisho yafanane na yaliyomo kwenye daftari hilo.