FM Manyara
FM Manyara
18 October 2025, 9:00 pm

Na Marino Kawishe
Zaidi ya shilingi Bilion mbili zimetekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika kata ya Gidas chini ya uongozi wa Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini kwa kipindi cha miaka minne iliyopita wakati huu wa uongozi wa Rais Samia Suluhu.
Akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa Hadhara wa kampeni kunadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Daniel Baran Sillo amesema bado Kuna changamoto chache zilizosalia ambazo akipata Ridhaa ya kuchaguliwa Katika uchaguzi utakaofanyika October 29 atazikamilisha kwa kipindi cha miaka mitano.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Babati Vijijini Jackson Haibey amewata wananchi kujitokeza kupiga kura kwani ni haki yao kikatiba kumchagua Rais, Mbunge na Diwani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika October 29 mwaka huu.
