FM Manyara
FM Manyara
16 October 2025, 9:07 pm

Na Marino Kawishe
Zaidi ya sh Bilion 1.4 zimewanufaisha wakulima Ishirini kutoka Wilayani Hanang ambao wamepatiwa Mkopo wa vifaa vya Kilimo ikiwemo Trekta kutoka kampuni ya Pass Leasing ambayo inafanya kazi na wakulima wengi hapa Nchini.
Akizungumza mbele ya Wananchi na wakulima waliojitokeza kwenye hafla ya ukabidhiwaji Trekta hizo Mgani rasmi ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Hanang Halmishi Hazari amewataka wanufaika wa mikopo hiyo ya trekta kuhakikisha wanaendela kuongeza tija kwenye kilimo ili kunufaika zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Pass Leasing Nchini Tanzania Killo Lusewa amesema mpaka sasa Kampuni hiyo imeshatoa vifaa vya Kilimo vyenye thamani ya Bilion sabini tangu kampuni hiyo izaliwe kutoka kwa Kampuni tanzu ya Pass Trust.
Aidha miongoni mwa wakulima waliopata mkopo wa Trekta na mgombea udiwan wa kata ya Gitting Marko Mamoya ameishukuru kampuni ya Pass Leasing na kusema sasa ataenda kuongeza ukubwa wa maeneo ya kilimo kutoka Ekari 30 alizolima sasa ili kuongeza tija kwenye kilimo hicho.
