FM Manyara

Siku ya kichaa cha mbwa yaadhimishwa kitaifa Kiteto

28 September 2025, 2:40 pm

Picha ya Mbwa

Siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani imeadhimishwa leo kitaifa wilayani Kiteto mkoani Manyara ambapo jamii imetakiwa kuwatunza mbwa na kuwapatia chakula cha kutosha ili kudhibiti tatizo la mbwa kuzurura.

Na Mzidalfa Zaid

Akizungumza na FM Manyara Daktari wa mifugo halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara Fatuma Mkombozi , amesema kupitia siku hii wametoa elimu kwa wafugaji pamoja na utoaji wa chanjo huku akielezea lengo la kuadhimishwa siku hii.

Sauti ya Daktari wa mifugo halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara Fatuma Mkombozi
Picha Daktari wa mifugo halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara Fatuma Mkombozi

Amesema huduma ya kwanza ambayo inatolewa kwa mtu anapong’atwa na mbwa mwenye kichaa cha mbwa anapaswa kunawa sehemu aliyong’atwa kwa maji safi yanayotiririka kisha kupelekwa hospitali ili afanyiwe matibabu.