FM Manyara

Mgombea Urais ADA TADEA awataka wananchi kusikiliza sera za wagombea

24 September 2025, 5:27 pm

picha ya Mgombea Urais Wa Jamuhuri ya muungano Wa Tanzania kutoka chama Cha ADA TADEA Georges Bussungu

Mgombea Urais Wa Jamuhuri ya muungano Wa Tanzania kutoka chama Cha ADA TADEA Georges Bussungu amewataka wananchi kufikia katika kampeini za wagombea mbalimbali na kusikiliza sera bila kuwa na hofu ya aina yeyote.

Na Diana Dionis

Bussungu ameyasema hayo wakati  alipokua akinadi sera zake kwenye mkutano Wa Kampeni uliofanyika Babati mjini mkoani Manyara, ambapo amewaasa wananchi kutokua na hofu ya kufika kwenye mikutano mbalimbali ya wagombea urais, ubunge na udiwani.

sauti ya Mgombea Urais Wa Jamuhuri ya muungano Wa Tanzania kutoka chama Cha ADA TADEA Georges Bussungu

Bussungu amesema endapo atapata ridhaa ya kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania watamachagua Waziri mkuu ambae ni msomi ambae atakuwa mtendaji mkuu  haijalishi anatokea chama kipi.