FM Manyara
FM Manyara
23 September 2025, 6:36 pm

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania(TMA)mkoa wa Manyara, imesema mvua za msimu zinatarajia kunyesha chini ya wastani hadi wastani ambapo wananchi mkoani Manyara wametakiwa kuzingatia utabiri huo.
Na Mzidalfa Zaid
Hayo yameelezwa na Meneja wa TMA mkoa wa Manyara Salma Amour, wakati akiongea na Fm Manyara, amesema mvua zitaongezeka kuanzia mwezi december.
Amewataka wananchi mkoa wa Manyara wakiwemo wakulima, wafugaji na wavuvi kufuatilia kwa ukaribu utabiri wa hali ya hewa unatolewa kwa masaa 24 ili kufanya shughuli zinazoendana na utabiri.
Kwa upande wake Hamimu Haji kutoka ofisi ya TMA mkoa wa Manyara, amesema utabiri huo unaelezea hali ambayo inatarajia kutokea katika mkoa wa Manyara.