FM Manyara
FM Manyara
3 September 2025, 7:01 pm

Jamii mkoani Manyara imetakiwa kuhakikisha watoto wote kuanzia umri wa miaka 0 hadi 8 wanapata lishe bora na huduma za malezi jumuishi ili iwasadie katika ukuaji .
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo umetolewa leo na mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Neema Kasabile ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikao cha kupitia utekelezaji wa shughuli za mpango wa MMMAM.
Amewataka maafisa maendeleo na maafisa ustawi wa jamii kuhakisha wanalinda usalama wa mtoto na kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuepukana na vitendo vya ukatili.
Nao baadhi ya washiriki wa kikao hicho, wameiomba jamii kuendelea kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa wanapoona vitendo vya ukatili wa kijinsia vikitendeka kwa watoto.
Aidha Afisa Mradi wa Mtoto Kwanza kutoka Shirika la COSITA Agustino Balohho, amesema suala la kupinga ukatili sio la serikali pekee bali ni la jamii yote kwa ujumla.
