FM Manyara
FM Manyara
21 August 2025, 4:33 pm

Serikali mkoani Manyara , imeelezea sababu zilizopelekea kushuka kwa bei ya Mbaazi , kufuatia kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wakulima wakilalamikia bei ya mbaazi kushuka na kuuzwa kilo moja kwa shilingi 800.
Na Mzidalfa Zaid
Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Manyara, Absalom Cheliga, amesema sababu ya kushuka kwa bei ya Mbaazi kwa kipindi hiki cha mwaka 2025 ni kutokana na nchi nyingi kulima zao la mbaazi kwa mwaka huu tofauti na mwaka uliopita.
Amewataka wakulima kuuza Mbaazi kupitia mfumo wa Stakabadhi Ghalani, kwakuwa unasaidia mkulima kuuza mbaazi kwa gharama kubwa tofauti na bei wanayouuza kwa walanguzi , ambapo amesema kwa minada iliyopita wameuza kilo ya mbaazi kwa shilingi 1010.
Awali baadhi ya wakulima, wameelezea namna bei hiyo inavyomkandamiza mkulima, na kusema malengo waliyojiwekea kwa mwaka huu hayatatimia kutokana na matarajio waliyoyatarajia.