FM Manyara
FM Manyara
24 July 2025, 6:42 pm

Na Mzidalfa Zaid
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amemwagiza mkandarasi ambaye amekabidhiwa mradi wa ujenzi wa stendi kuu ya mabasi mkoa wa Manyara, kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo kwa wakati ili ianze kutumika na wananchi wanufaike na mradi huo.
Sendiga ametoa agizo hilo katika hafla ya kumkabidhi mkandarasi mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi na barabara za lami na mitaro. Ameongeza kuwa mradi huo uwe umekamilika ndani ya miezi 15.
Akitoa taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Shaaban Mpendu, amesema mradi huo utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 19.9 ambapo amesema watasimamia mradi huo ili ukamilike kwa wakati.
Kwa upande wake mkandarasi ambaye amekabidhiwa mradi huo Kisirieri Werema amesema watafanya kazi usiku na mchana ili mradi huo ukamilike, na wataanza kazi baada ya vibanda vilivyopo stendi kuondolewa.
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mhe. Paulina Gekul, amesema ni kwa muda mrefu amekuwa akiiomba serikali kutengeneza stendi hiyo ambapo ameishkuru serikali ya awamu ya sita kwa kutenga fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa stendi hiyo ya kisasa.