FM Manyara
FM Manyara
18 July 2025, 5:15 pm

Waandishi wa habari mkoani Mmanyara wamepatiwa mafunzo ya kujengewa uwezo wa kufanya shughuli zao za kuelimisha jamii zinazohusu habari za ukaguzi.
Mafunzo hayo yametolewa na wataalamu kutoka Tasisi ya mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) kwa lengo la kuwawezesha waandishi wa habari kufikisha taarifa na elimu sahihi kwa jamii zinazohusu ukaguzi.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini Focus Mauki amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuhakikisha ripoti zaCAG zinafikia umma kupitia kwa waandishi wa habari ambao wanaweza kufikia watu wengi kwa pamoja.
Kwa upande wake mkaguzi mkuu wa nje mkoa wa Manyara Mary Dibogo amesema matumizi ya Tehama yamerahisisha kupatikana kwa taarifa za ubadhirifu ambazo zitamsaidia CAG kufanya kazi zake katika maeneo husika.

Akiongea kwa niaba ya mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Manyara, katibu wa chama hicho Jaliwason Jasson, amesema walituma maombi kwa ofisi ya mkaguzi ili watoe elimu kwa wanahabari wapate ufahamu wa habari za ukaguzi.