FM Manyara
FM Manyara
18 July 2025, 4:57 pm

Mwenge wa uhuru umezindua mradi wa tenk la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita million mbilis lenye thamani ya zaidi ya shilingi billion 41 katika wilaya ya Mbulu kwakua itasaidia kuondokana na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama kwa wananchi katika kijiji hicho.
Na Emmy Peter
Akizungumza baada ya kuzindua mradi huo kutoka wakala wa maji vijijini na usafi wa mazingira Ruwasa , mkimbiza mwenge wa uhuru kitaifa Ismaili Ally Ussi amesema sekta ya maji imekuwa ikitekeleza miradi katika kuzingatia ubora wa huduma ya maji safi na salama kwa mwananchi ambapo amewataka wananchi kuendelea kutunza miundombinu ya maji katika maeneo yao.
Kwa upande wake Meneja wa Ruwasaa mkoa wa Manyara mhandisi James Kionaumela amesema mradi huo utahudumia vijiji 21 pamoja na wananchi zaidi ya laki moja kunufaika na mradi huo wa maji ambapo amesema hadi sasa wamechimba visima 3 na upatikanaji wa maji utakuwa wa uhakika.