FM Manyara

DC Kaganda awataka waandishi wa habari kukemea ukatili

13 July 2025, 11:39 pm

Picha ya mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda

Mkuu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara Emmanuela Kaganda, amewataka waandishi wa habari mkoani Manyara kuendelea kuibua na kuripoti matukio ya kikatili ili wahusike wachukuliwe hatua kali za kisheria na vitendo hivyo vidhibitiwe .

Na Mzidalfa Zaid

Kaganda ametoa kauli hiyo leo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake, amevipongeza vyombo vya habari kwa kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo vya ukatili  ikiwemo ubakaji, ukeketaji, matukio ya kujeruhi pamoja na matukio mbali mbali ya kikatili.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara Emmanuela Kaganda

Katika hatua nyingine , amekemea vitendo vya uharifu, amesema vyombo vya habari vimesaidia kukemea matukio hayo na kupelekea serikali ya wilaya kuchukua hatua za haraka za kudhibiti matukio ya kiuharifu.

Aidha, amesema ofisi ya mkuu wa wilaya ya Babati, itaendelea kushirikiana na waandishi wa habari wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao, ambapo amewataka waandishi wa habari wasisite kutoa taarifa za kuisaidia jamii.