FM Manyara
FM Manyara
13 July 2025, 11:04 pm

Zaidi ya wanachi 3,000 Katika Kijiji cha Nadonjukin wilaya ya simanjiro Mkoani Manyara wameondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta Maji baada ya Mwenge wa Uhuru kuzindua mradi wa Maji kutoka RUWASA uliogharimu zaidi ya Shilingi Million miasita.
Na Emmy Peter
Akizungumza baada ya uzinduzi wa Mradi huo kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Ismaili Ally Ussi Ameipongeza Ruwasa kwa kuwa na Miradi ya kisasa inayo leta tija Kwa wananchi
Kwa upande wake Meneja wa wakala wa Maji na usafi wa mazingira vijijini(RUWASA) mkoa wa Manyara Injinia James Kiunaumela ameeleza mafanikio ya Miradi hiyo kwa wananchi, na kusema Ruwasa mkoa wa Manyara wamefika asilimia 78.9 kwa kuwafikishia huduma ya Maji safi na salama wananchi wa mkoa wa Manyara.
Aidha wananchi Wa Kijiji cha Nadonjukin wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan Kwa kuwaletea Mradi huo wa Maji kutoka Ruwasa kwani imesaidia kutatua changamoto iliyokuwa ikiwakabili kwa Muda Mrefu.