FM Manyara

Sigino yatumia 2.5b za miradi ya maendeleo

1 July 2025, 11:17 am

Picha za wananchi wa kata ya sigino wakisikiliza na kutoa changamoto zao kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati

Ziara ya Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara ya kuueleza mafanikio ya serikali ya awamu ya sita na kusikiliza kero za wananchi imeendelea leo katika kata ya Sigino.

Na George Augustino.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati Mkoa wa Manyara CPA Shaaban Mpendu amesema kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2025 kata ya Sigino imepokea na kutumia kiasi cha shilingi billioni mbili na nusu katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza leo katika ziara yake ya kata kwa kata kueleza mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa awamu ya sita ya Rais Samia Suluh Hasani CPA Mpendu amesema fedha hizo zimetumika katika miradi ya elimu, afya, kilimo na mifugo, TASAF pamoja na mikopo ya vijana ,wanawake na watu wenye mahitaji maalum.

Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa ababati

Aidha CPA Mpendu amesikiliza kero na changamoto za wananchi wa kata ya Sigino pamoja na kutatua changamoto hizo na kuzijibu kwakushirikiana na wakuu wa idara mbalimbali wa halmashauri hiyo na taasisi nyingine za serikali waliokuwepo katika mkutano huo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa ababati

Aidha amewataka wananchi wa Sigino kuchangamkia mikopo inayotolewa na Halmashauri kwaajili ya vijana wanawake na watu wenye mahitaji maalumu ili kunufaika nayo na kujikwamua kiuchumi .