FM Manyara
FM Manyara
20 June 2025, 9:59 pm

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati Shaaban Mpendu amefanya ziara ya kikazi katika kata ya bonga na kusikiliza changamoto za wananchi wa kata hiyo pamoja na kutoa takwimu ya fedha na miradi iliyotekelezwa.
Na George Augustino.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara Shaaban Mpendu ametoa takwimu ya fedha zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani kwa ajili ya maendeleo ya kata ya Bonga kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi mwaka 2024/2025.
Akitoa takwimu hiyo leo katika mkutano uliofanyika katika kata ya Bonga na kuhudhuriwa na wananchi wa kata hiyo pamoja na wataalam mbalimbali wa halmashauri hiyo Mpendu amesema fedha za maendeleo zilizopokelewa na kutumika katika maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo elimu na afya ni zaidi ya shilingi billioni mbili .
Aidha Mpendu pamoja na wataalamu wa idara mbalimbali za halmashauri amesikiliza changamoto na kero za waanchi wa kata hiyo ikiwemo changamoto ya mikopo inayotolewa na halmashauri kwa vijana wanawake na watu wenye ulemavu ,tatizo la kuunganishiwa umeme, choo cha soko pamoja na dampo la taka .
Aidha changamoto hizo zilizotolewa na baadhi ya wananchi wa kata ya bonga zimetolewa majibu na kupatiwa ufumbuzi na mkurugezi wa halmashauri ya mji wa babati pamoja na wakuu wa idara malimbalimbali wa halmashauri hiyo.