FM Manyara

Wafanyabiashara wa mazao ya misitu, nyuki watakiwa kujisajili

19 June 2025, 11:14 pm

picha ya kaim mhifadhi wa mistu TFS wilaya ya Hanang mkoani Manyara Abubakari Mpapa

Wafanyabiashara wa mazao ya misitu na mazao ya nyuki wilayani Hanang mkoani Manyara wametakiwa kujisajili kupata leseni za kufanya biashara hizo au kuuisha leseni zao kwa wafanyabiashara ambao wana leseni ifikapo july 1.

Na Mzidalfa Zaid

Wito huo umetolewa na kaim mhifadhi wa mistu TFS wilaya ya Hanang mkoani Manyara Abubakari Mpapa wakati akiongea na fm Manyara, amesema kabla na  baada ya mwaka fedha, wamekuwa wakiendesha zoezi la uishaji na usajili wa leseni za mazao ya misitu na nyuki  ili wafanyabiashara hao wafanye biashara hizo kwa uhuru.

Amewaonya wafanyabiashara  ambao wamekuwa wakifanya biashara za mazao ya mistu na mazao ya nyuki  pasipokufuata utaratibu waache mara moja kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Sauti ya kaim mhifadhi wa mistu TFS wilaya ya Hanang mkoani Manyara Abubakari Mpapa

Aidha amesema wamekuwa wakitoa elimu mbalimbali kwa wanananchi inayohusu umuhimu wa kujisajili kupitia vyombo vya habari , mitandao ya kijamii pamoja na maeneo yenye mikusanyiko.