FM Manyara
FM Manyara
19 June 2025, 10:49 pm

Wananchi wa kata ya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara, wameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuleta maendeleo katika kata hiyo kwa kuhakikisha inatatua changamoto ya maji, afya, bara bara, elimu na kilimo huku wakimpongeza diwani wa kata hiyo kwa kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
Na Mzidalfa Zaid
Wananchi hao wametoa pongezi hizo leo baada ya kusomewa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kwa kipindi Cha miaka mitano kuanzia 2020/2025 .
Awali afisa elimu kata Magugu Ally Msuya ambae amemuwakilisha afisa mtendaji wa kata hiyo, ameelezea utekelezaji wa chama cha mapinduzi kwa miaka mitano, ambapo amesema katika kipindi hicho serikali imefanikia kutatua changamoto ya maji, bara bara na sekta mbalimbali.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Magugu Filbert Modamba ameelezea namna alivyojitoa katika kipindi chote cha uongozi na kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.