FM Manyara

Sendiga aboresha taarifa zake katika daftari la kudumu la mpiga kura

22 May 2025, 3:27 pm

Picha ya Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Wananchi mkoani Manyara ambao hawajaboresha taarifa zao wametakiwa kufika kwenye vituo vilivyopangwa kwa ajili ya kuboreshe taarifa zao kwa muda uliobaki ili kupata fursa ya kushiriki Uchaguzi Mkuu  unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.

Na Mzidalfa Zaid

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendiga ameboresha taarifa zake katika Daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili katika kituo cha Ofisi ya kata ya Babati Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.

Akizungumza baada ya kuboresha taarifa zake, amewataka wananchi ambao hawajaboresha taarifa zao wafike kwenye vituo vilivyopangwa ili waboreshe taarifa hizo kwa muda ambao umebaki ili kupata fursa ya kushiriki Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendiga

Kwa upande wake afisa uandikishaji jimbo la babati mjini Edina Moshi, amesema hadi kufikia jana , katika jimbo la babati mjini wameandikisha wapiga kura wapya 1294 , na watu 1599 wameboresha taarifa zao na majina ya wananachi 498 yamefutwa kutokana na vifo.

Sauti ya afisa uandikishaji jimbo la babati mjini Edina moshi,

Aidha,baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kuborehsa taarifa zao, wamesema lengo la kuboresha taarifa hizo ni kushiriki uchaguzi mkuu na kumchagua kiongozi wanaemtaka.

Sauti ya baadhi ya wananchi