FM Manyara
FM Manyara
21 May 2025, 6:03 pm

Wanafunzi wa shule ya msingi Ayamango iliyopo kwenye kijiji cha ayamango kata ya Galapo wilayani Babati mkoani Manyara wamejengewa miundombinu ya kisasa ya vyoo vya wanafunzi na walimu baada ya choo cha zamani kutitia na kuleta hatari ya magonjwa ya mlipuko
Na Marino Kawishe
Shirika lisilo la kiserikali la SO THEY CAN Tanzania limewaunga mkono wananchi wa kijiji cha Ayamango kilichopo kata ya Galapo wilayani Babati mkoani Manyara ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindu pindu kwa kuwajengea miundombinu ya kisasa ya vyoo wanafunzi wa shule ya msingi Ayamango.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa vyoo hivyo mbele ya naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Daniel Sillo,Meneja mkazi wa shirika hilo Roselyne Mariki amesema ujenzi huo umekwenda sambamba na ujenzi wa kisima cha maji pamoja na tank lenye uwezo wakubeba lita elfu 30.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya msingi Ayamango Baraza Shana amesema mradi huu ni muhimu na utaboresha afya za wanafunzi zaidi ya 500 na mazingira ya wananchi wanaoishi pembezoni mwa shule hiyo.
