FM Manyara
FM Manyara
16 May 2025, 4:47 pm

Shirika la So They Can Tanzania (STC) limesema kwa miaka mitano iliyopita licha ya changamoto kadhaa kwenye maeneo ya mradi wanakofanya kazi bado kumekuwepo mafanikio makubwa ambayo yanawafanya kuendelea kutanua wigo wake kwa miaka mitano ijayo.
Na Marino Kawishe
Akizungumza na Fm Manyara kwenye mahojiano maalumu ya utekelezwaji mpango huo Meneja mkaazi wa shirika la So They Can Tanzania Roselyne Mariki amesema mpango wa miaka mitano uliopita ulilenga uboreshaji miundombinu ya mashule, mafunzo ya waalimu wakujitolea na masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto pamoja na shamba letu.
Ameongeza kuwa kwa miaka mitano iliyopita wameweza kufikia malengo na kuongeza idadi ya wanafunzi kupata elimu kutoka mazingira magumu na ufaulu kupanda katika kata za mradi.
Aidha Meneja huyo ametoa pongezi kwa Serikali ya halmashauri ya Wilaya ya Babati pamoja na mashirika mengine walioshirikiana kwa pamoja kutekeleza mipango hiyo bila kuwasahau wananchi walioshiriki kwa nguvu zote kuhakikisha miradi ya shirika hilo inasima.
Kwa upande wao maafisa Elimu maalumu na kata wamelishukuru shirika la so they Can kwa kuguswa na kuwekeza kwenye elimu kwani wameweza kuhamasisha upatikanaji wa chakula katika shule za msingi na sekondari na kuendelea kutoa elimu ya masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto kwenye kata ambazo mradi huo umetekelezwa.
