FM Manyara

EWURA yawahimiza wananchi kutumia nishati safi ya kupikia

16 May 2025, 4:34 pm

picha ya Meneja wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA) kanda ya kaskazini lorivii lon’gidu

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA) kanda ya kaskazini imewataka wananchi kutumia nishati safi ya kupikia majumbani maarufu kama (LPG) na kuachana na matumizi ya mkaa na kuni .

Na Mzidalfa Zaid

Wananchi mkoani Manyara na kanda ya kaskazini kwa ujumla, wametakiwa kutumia nishati safi ya kupikia majumbani maarufu kama (LPG) na kuachana na matumizi ya mkaa na kuni .

Wito huo umetolewa leo na Meneja wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA) kanda ya kaskazini lorivii lon’gidu alipokuwa akiongea na fm manyara, amesema mkakati wa seikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2034 zaidi ya asilimia 80 ,Gas ya majumbani iwe imewafikia wananchi majumbani.

sauti ya Meneja wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA) kanda ya kaskazini lorivii lon’gidu

Aidha, amesema muitikio wa wananchi kutumia Gas umekuwa mkubwa kutokana na tathmini ya miaka kumi iliyopita, wananchi wengi walikuwa hawatumia Gas tofauti na kipindi hiki ambacho wananchi wengi wanatumia Gas.