FM Manyara

BASATA yawataka wasanii kujisajili

16 May 2025, 3:33 pm

Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kujisajili ili kutambuliwa na Baraza hilo ili wafanye shughuli hizo kwa ufasaha

Na Mzidalfa Zaid

Wasanii mkoani Manyara na nchini kwa ujumla wametakiwa kujisajili katika Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ili kutambuliwa na Baraza hilo na kupatiwa cheti cha sanaa pamoja na kupata fursa zitokanazo na sanaa .

Afisa kutoka BASATA Filipo Mkemwa, amesema hayo wakati akiongea na fm Manyara , amesema kila msanii anapaswa kujisajili ili kutambuliwa na Baraza hilo ili awe na uhuru wa kufanya kazi sehemu yeyote ndani na nje ya nchi.

Sauti ya Afisa kutoka BASATA Filipo Mkemwa

Kwa upande wake afisa sanaa kutoka BASATA Dalianus Mtembei amesema kuna makundi matatu ambayo yanatambuliwa na BASATA ikiwemo sanaa ya muziki, sanaa ya ufundi , na sanaa ya maonyesho ambapo amesema kwa sasa Taasisi hiyo imeendelea kuboresha mifumo ya usajili kupitia online popote alipo na mfumo kumtambua alipo na sanaa anayo ifanya.

Sauti ya afisa sanaa kutoka BASATA Dalianu