FM Manyara

TAKUKURU Manyara  yaokoa zaidi ya shilingi milioni 300

13 May 2025, 6:49 pm

picha ya mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Adam Mbwana

Kaim Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Adam Mbwana, amesema TAKUKURU mkoa wa Manyara imeokoa zaidi ya  shilingi milioni 300 kwa kipindi cha janaury -march

Na Mzidalfa Zaid

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Manyara imeokoa zaidi ya shilingi milioni 300 kwa kipindi cha january hadi march mwaka huu baada ya TAKUKURU kufanya uchunguzi.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake, kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Adam Mbwana, amesema TAKUKURU imeokoa zaidi ya  shilingi milioni 260 kutoka kwa wawekezaji waliopangisha katika hifadhi ya wanyamapori Burunge ambayo ni fedha ya kodi ya kupangisha katika hifadhi inayopaswa kugawanya kwa vijiji husika.

sauti ya kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Adam Mbwana

Katika hatua nyingine amesema katika kipindi hicho TAKUKURU mkoa wa Manyara ilipokea malalamiko 105 na kati ya hayo malalamiko 78 yalihusu rushwa , 27 hayakuhusu rushwa na kesi 15 zilifunguliwa mahakamani na kesi 8 zinaendelea mahakamani.

sauti ya kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Adam Mbwana

Aidha, amewataka wananchi mkoani Manyara kuendelea kutoa taarifa TAKUKURU wanapobaini viashiria vyovyote vya rushwa ili hatua kali zichukuliwe kwa wahusika.