FM Manyara

Qash Sekondari yakabidhiwa bweni lenye thamani ya shillingi million 200

13 May 2025, 6:30 pm

Mkurugenzi mkazi wa Shirika la STC Roselyne Mariki amesema ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Qash umegharimu kiasi cha shilingi million mia mbili na limejengwa kwa ushirikiano wa wananchi wa kata ya Qash

Na Marino Kawishe

Shirika lisilokuwa la Kiserikali la STC limekabidhi  mbweni moja lenye thamani ya shillingi million mia mbili kwa shule ya sekondari ya Qash iliyopo wilayani Babati mkoani Manyara lenye uwezo wakukaa wanafunzi 80 wa kike.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa bweni hilo mkurugenzi mkazi wa Shirika la STC Roselyne Mariki amesema ujenzi wa bweni hilo pamoja na thamani zilizowekwa umegharimu kiasi cha shilingi million mia mbili na limejengwa kwa ushirikiano wa wananchi wa kata ya Qash ambao wamechangia asilimia saba ya ujenzi huo.

sauti ya mkurugenzi mkazi wa Shirika la STC Roselyne Mariki

Kwa upande wake Naibu waziri wa Mambo ya ndani na mbunge wa jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo amesema mazingira mazuri ya Uwekezaji yaliyowekwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr samia Suluhu Hassan imepelekea wawekezaji kuendelea kuwekeza kwenye maeneo mbali mbali hapa nchini.

sauti ya Naibu waziri wa Mambo ya ndani na mbunge wa jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo

Aidha Wananchi wa kata ya Qash wamelishukuru shirika la STC kwa kuwezesha kukamilika mbweni hilo nakuomba waendelee kuwashika mkono Wananchi hao hata katika miradi mingine.

sauti ya Wananchi wa kata ya Qash

Aidha,mradi huo wa bweni la wasichana ni sehemu ya utekelezaji miradi mbali mbali ya shirika hilo ambalo limeendelea kukamilika katika kata nne za mradi ambazo ni Qash, Galapo, Endakiso na Mamire zilizopo Wilayani Babati mkoani Manyara.