FM Manyara
FM Manyara
7 May 2025, 5:38 pm

Bei mpya ya mafuta imeanza kutumika leo Mei 7, 2025 na mabadiliko hayo yametokana na mabadiliko ya bei katika soko la dunia ambapo bei ya petrol imepungua kwa shilingi 89 na bei ya disel ni shilingi 68.
Na Mzidalfa Zaid
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA) kanda ya kaskazini imetangaza bei mpya ya mafuta ambayo imeanza kutumika leo may 7 2025 ambapo bei ya mafuta kwa kanda ya kaskazini imeshuka ikilinganishwa na mwezi april.
Meneja wa EWURA kanda ya kaskazini Lorivii Long’idu, ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea kwa njia ya simu na fm Manyara,amesema bei mpya imeanza kutumika leo na mabadiliko hayo yametokana na mabadiliko ya bei katika soko la dunia ambapo bei ya petrol imepungua kwa shilingi 89 na bei ya disel ni shilingi 68 huku bei ya mafuta ya taa ikibakiwa kama ilivyokuwa mwezi april.
Aidha, amewataka wananchi mkoani Manyara na kanda ya kaskazini kwa ujumla kutoa taarifa EWURA wanapouziwa mafuta kwa bei ya juu zaidi tofauti na ile iliyotangazwa na ewura na akiwataka wafanyabiashara wa mafuta kuhakikisha wanauza mafuta kwa bei elekezi.