FM Manyara

Wakulima Manyara watakiwa kuacha kutegemea kilimo cha mvua

7 May 2025, 12:56 pm

Meneja kutoka shirika la Kickstart Ernest Jerome aelezea jinsi kilimo cha umwagiliaji kilinavyoweza kumwinua mkulima mdogo na mkubwaa kwa kutumià vifaa ambavyo vitamwezesha mkulima kumwagilia kwa urahisi.
 
 
 Na Angel Munuo
 
Wakulima mkoani Manyara wametakiwa kuacha kutegemea kilimo cha mvua pekee na badala yake kulima kilimo cha umwagiliaji ili kupata mazao ya uhakika na  kujiongezea kipato.
 
Wito huo umetolewa na meneja kutoka shirika la kickstart Ernest Jerome alipokuwa akitoa elimu kwa wakulimà wa mkoa wa Manyara jinsi kilimo cha umwagiliaji kilinavyoweza kumwinua mkulima mdogo na mkubwaa kwa kutumià vifaa ambavyo vitamwezesha mkulima kumwagilia kwa urahisi.

Sauti ya meneja kutoka shirika la kickstart Ernest Jerome

kwa upande wake  mwakilishi kutoka ofisi ya mkoa wa manyara Magreth wiza aliyekuwa mgeni rasmi,amesema kuna haja ya wakulimà kuvuna maji kipindi cha mvua ili kulima kilimo cha umwagiliaji hususani  msimu wa kiangazi na kuacha kutegemea mvuaa ambayo haitoi matokeao mazuri katika kilimo kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

sauti ya mwakilishi kutoka ofisi ya mkoa wa manyara Magreth wiza

Aidha,wakulimà hao wamelipongeza shirika hilo  kwa kuwapa elimu kuhusu kilimo cha umwagiliaji ambacho kitawasaidia kupata mazao ya uhakika katika misimu yotee na wataweza kujiongezea kipato kutokana na kilimo cha umwagiliaji.

sauti ya wakulima