FM Manyara

Sillo awaasa wananchi Babati kushiriki uchaguzi mkuu Oktoba 2025

6 May 2025, 5:39 pm

Naibu Waziri Sillo akihutubia wananchi Kifaru juu

Serikali ya awamu ya sita kwa kushirikiana na taasisi ya Karimu Foundation na shirika lisilokuwa la Kiserikali la So They Can Tanzania (STC) imefanikisha miradi mbali mbali ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa vituo vya fya.

Na Marino kawishe

Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya nchi na mbunge wa jimbo la Babati Vijijini  Daniel Sillo  amewaasa wananchi wa kitongoji cha Kifaru juu kata ya Endakiso wilayani Babati mkoani Manyara kushiriki kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi October mwaka huu. 

Sillo amezungumza na wananchi wa kitongoji hicho wakati wa ufunguzi wa vyoo vya kisasa vilivyojengwa na Taasisi ya Karimu Foundation kwa ushirikiano na shirika la STC amesema serikali ya awamu ya sita imefanikisha miradi mbali mbali ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa vituo vya fya.

sauti ya Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya nchi na mbunge wa jimbo la Babati Vijijini  Daniel Sillo 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya karimu Foundation  Shao Erri amesema wataendelea kusaidia jamii hasa kwenye maeneo ya miradi yao ambayo imekuwa na changamoto mbali mbali. 

sauti ya Mkurugenzi wa taasisi ya karimu Foundation  Shao Erri

Aidha,mradi huo wa vyoo vya kisasa umegharimu zaidi ya shilingi milion 100 ambapo  taasisi hiyo  imechangia zaidi ya milion 80 na  ofisi ya mbunge imechangia milion 2 nawananchi wa kitongoji cha kifaru juu wakichangia kiasi kilichobaki.