FM Manyara

Semi yaziba njia na kusababisha foleni barabara ya Galapo-Babati

11 April 2025, 6:39 pm

Gari kubwa aina ya semi limesasabisha foleni baada kusimama katikati ya barabara na kusababisha magari kushindwa kupita kutokana na ubovu wa barabara baada ya mvua kunyesha wilayani babati mkoani Manyara

Na Mzidalfa Zaid

Wananchi wanaotumia Barabara ya Babati Galapo wilayani Babati mkoani Manyara leo april 11.2025  asubuhi wamekumbwa na adha ya foleni kubwa baada ya gari kubwa aina ya semi kusimama katikati ya barabara na kusababisha magari kushindwa kupita .

Wakizungumza na  fm Manyara wananchi ambao wamekumbwa na adha hiyo wamesema zaidi ya magari 20 yamekwama baada ya barabara hiyo kushindwa kupitika kuanzia majira ya saa moja asubuhi hadi saa tano asubuhi.

Awali  baada ya ya fm manyara radio kupata taarifa hiyo ilimtafuta kamanda wa usalama Barabarani MichaelMwakasungula  na kuahidi kufatilia ili kutatatua changamoto hiyo.