FM Manyara

ALAT yakagua majengo mapya ya hospitali ya mji wa Babati

8 March 2025, 12:52 am

Kamati ya Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mkoa wa Manyara imefanya ukaguzi wa miradi katika halmashauri ya mji wa Babati.

Na Mzidalfa Zaid

Kamati ya Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mkoa wa Manyara imekagua majengo mapya ya hospitali ya mji wa  Babati (Mrara)  yenye Thamani ya shilingi bilioni 1.4.

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi huo mwenyekiti wa kamati hiyo Peter Sulle amepongeza halmashauri ya mji Babati Kwa kusimamia vyema Mradi huo na kukamilika Kwa wakati ambapo ameuagiza uongozi wa halmashauri ya Babati mji kuweka CCTV camera Ili huduma zitolewe Kwa ufasaha.

Amesema kukamilika Kwa majengo Hayo Kwa wakati kumetokana  na Ufatiliaji Wa karibu pamoja na ushirikiano Kati ya ofisi ya Halmashauri na ofisi ya mkuu wa wilaya Babati.

Kwa upande wake Mkurugenzi Wa halmashauri ya mji babati Shaban mpendu amesema ujenzi wa majengo ya hospitali  ya mji Babati Mrara Kwa sasa umefikia asilmia 98 na wanatarajia kuanza kutoa huduma kwenye majengo Hayo mwishomi mwa wiki hiii Kwa kuwa Vifaa vyote vimekamilika na kusema changamoto zilizokuwepo awali zimefanyiwa kazi.

Sauti ya Mkurugenzi Wa halmashauri ya mji Babati Shaban mpendu

Nae Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Babati Nasibu Msuya amesema watahakikisha wanasimamia huduma Bora hospitalini hapo na kuondoa malalamiko Kwa wateja na wameanzisha kundi sogozi Kwa ajili ya kuwapa fursa wananchi kutoa maoni na malalamiko yao kupitia kundi Hilo.

Sauti ya Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Babati Nasibu Msuya

Baadhi ya wajumbe WA kamati hiyo  wakiwa kwenye hospitali hiyo ya mji babati Mrara wamefurahishwa na utekelezaji wa ujenzi huo na kutaka huduma zitakazo tolewa kuwa Bora zaidi Kwa kujali wanao hudumiwa ili kuondoa malalamiko.