

20 February 2025, 11:03 pm
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Cuthbert Sendiga, ameongoza hafla ya kilele cha siku ya mlipa kodi.
Na Mzidalfa Zaid
Mkuu wa mkoa wa manyara Queen Sendiga amewaonya baadhi wafanyabiashara ambao wamekuwa hawatoi risiti au kutoa risiti ambazo haziendani na thamani ya mauzo hali inayokwamisha zoezi la ukusanyaji wa kodi .
Sendiga amesema hayo leo katika kilele cha siku ya mlipa kodi ambacho kimeambatana sambamba na pongezi kwa walipa kodi , amesema kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa sio wazalendo kwa kufanya udanganyifu wanapotembelewa na maafisa wa tra ambapo ameitaka jamii kutoa taarifa wanapowaona wafanyabiashara wa namna hiyo.
Kwa upande wake mwakilishi wa Kamishna wa TRA Nchini Hashim Ngoda, amesema mamlaka ya mapato tanzania(TRA) inashirikiana na wafanyabiashara kuhakikisha inalinda biashara zao na wameunda timu maalum inayotembelea wafanyabiashara kwenye maeneo yao na kutoa elimu kuhusu ulipaji wa kodi.
Meneja wa TRA Mkoa wa Manyara Alex Katundu, akisoma taarifa za Mkoa amesema Mkoa wa Manyara umevuka lengo la ukusanyaji wa kodi na hii ni kutokana na elimu ambayo wamekuwa wakiitoa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa ulipaji wa kodi kwa kuwa kodi hizo zimesaidia kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za Mkoa wa Manyara.