FM Manyara

Aliyekuwa mhasibu wa zahanati ya Endanachani afikishwa mahakamani

23 January 2025, 6:36 pm

Aliyekuwa mhasibu msaidizi katika zahanati ya Endanachani wilayani Babati mkoani Manyara Mohamed Baya amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Babati na kusomewa mashtaka 52.

Na Mzidalfa Zaid

Aliyekuwa mhasibu msaidizi katika zahanati ya Endanachani wilayani Babati mkoani Manyara Mohamed Baya mwenye umri wa miaka 33 amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Babati na kusomewa mashtaka 52.

Akisoma shauri hilo mbele ya hakim mkazi mkuu wa mahakama ya wilaya ya Babati Karim Mush, mwendesha mashtaka wa TAKUKURU wakili Martini Makani amesema mshitakiwa amefikishwa mahakamani hapo kwa makosa aliyoyatenda kati ya mwaka 2022/2023.

Mwendesha mashtaka Martini Makani, amesema mtuhumiwa huyo alitenda makosa 52 likiwemo la uhujum uchumi, utakatishaji fedha haramu na kugushi nyaraka na kujipatia fedha kwa nyakati tofauti kiasi cha shilingi milioni arobaini na nane na elf tisini.

Aidha kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena February 5 2025 na mtuhumiwa amepelekwa rumande kwa kuwa kosa la pili la utakatishaji fedha halina dhamana.