FM Manyara

Wananchi  Babati walalamika taka kutokuzolewa kwa wakati

9 January 2025, 4:30 pm

picha ya kizimba cha taka Babati

Wafanyabiashara katika eneo la Machinga complex lililopo mjini Babati mkoani Manyara wameiomba serikali ya halmashauri ya mji wa Babati kuondoa taka zilizojaa katika kizimba cha kuhifadhi taka

Na George Agustino

Wafanyabiashara katika eneo la Machinga complex lililopo mjini Babati mkoani Manyara wameiomba serikali ya halmashauri ya mji wa Babati kuondoa taka zilizojaa katika kizimba cha kuhifadhi taka kilichopo karibu na soko kuu la Babati kwani zinatoa harufu kali nakusababisha kushindwa kufanya biashara kwa amani.

Wafanyabiashara hao wametoa malalamiko hayo wakati wakizungumza na fm Manyara ambapo wamesema kwa mda mrefu taka hizo kutoka soko kuu na maeneo ya jirani zinapofanyika biashara hazijaondolewa katika eneo hilo na kupelekwa katika jalala kuu ambapo zimekuwa zikitoa harufu kali hali ambayo inaweza iksababisha kutokea kwa magonjwa ya mlipuko.

sauti za wafanyabiashara

kufuatia malalamiko hayo ya wafanyabiashara fm Manyara imezungumza na bibi afya wa kata ya Babati Mariamu Msangi amesema taka hizo hazijaondolewa kwa mda mrefu sababu gari la kuzoa taka lipo katika matengenezo na kusababisha taka hizo kutotolewa kwa wakati na kujaa katika kizimba hicho.

sauti ya bibi afya wa kata ya Babati Mariamu Msangi