Akutwa amefariki akiwa ndani kwake
20 December 2024, 12:50 am
Kufuatia kifo cha mwanamke aliyekutwa amefariki akiwa ndani kwake ndugu wa marehemu wasema ndugu yao hakuwa anaumwa zaidi alikuwa anasumbuliwa na kifua ambacho kilikuwa kinambana mara chache
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Anna Sanka mwenye umri wa miaka 47 kutoka kijiji cha mapea kata ya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara amekutwa amefariki usiku wa kuamkia leo december 19 nyumbani kwake.
Na hawa Rashid
Akiongea na Fm Manyara ndugu wa marehemu Rehema Sanka amesema jana alikuwa na dada yake na waliachana vizuri hakuwa anaumwa lakini leo asubuhi December 19 2024 alikwenda nyumbani kwa dada yake alikuta mlango upo wazi na dada yake akiwa amelala chali chini ameshafariki
Kwaupande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Mapea Juma Rashid amekiri kutokea kwa tukio hilo nakusema asubuhi ya leo december 19 2024 alipigiwa simu na mwenyekiti wake wa kitongoji cha msimbazi Maulid Juma akimwambia kunatukio limetokea katika kijiji chake ambapo walifika katika eneo la tukio nakujiridhisha ambapo walitoa taarifa kituo cha polisi kuhusu tukio hilo ambapo askari walifika na kuchunguza tukio hilo.
Aidha juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara zinaendelea ili kuthibitisha tukio hilo na kuelezea kwa undani