DC Kaganda azindua Mati Foundation
23 November 2024, 8:13 pm
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Mati Foundation yenye lengo la kusaidia wenye uhitaji na makundi maalumu ikiwemo wenye ulemavu iliyoko chini ya kampuni ya Mati Super Brands Limited imezinduliwa rasmi leo na Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda.
Na Mzidalfa Zaid
Akizungumza mara baada ya kuzindua Taasisi ya Mati Foundation, Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda amempongeza Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd David Mulokozi kwa kuisaidia jamii inayomzunguka katika Wilaya ya Babati na Tanzania kwa ujumla kwa kutoa sehemu ya faida anayoipata kusaidia jamii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Mati Foundation ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa ndoto yake ni kunyanyua jamii inayomzunguka kwa kurudisha sehemu ya faida anayoipata kwa jamii jambo ambalo limekuwa ni utamaduni wao na ibada pia.
Amesema kampuni hiyo imekuwa ikiunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi kupitia misaada mbali mbali wanayoitoa kwa jamii ya Watanzania.
Nae Mwenyekiti Msaidizi wa Mati Foundation Gwandumi Mpoma amesema kuwa wamekua wakitoa misaada sehemu mbali mbali ikiwemo kwenye maaafa ya Mafuriko hanang,kusaidia fimbo nyeupe kwa wenye ulemavu wa macho pamoja na kutoa misaada kwa yatima,wajane na wazee.
Amesema wametumia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 1.5 kusaidia jamii inayowazunguka kama mchango wao kwa jamii tangu kiwanda cha Mati Super Brands Limited kilipoanzishwa mwaka 2017.
Amesema kampuni hiyo imekuwa ikiunga mkono juhudi za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi kupitia misaada mbali mbali wanayoitoa kwa jamii ya Watanzania.