Manyara kuanzisha kliniki ya madaktari bingwa
18 November 2024, 9:00 pm
Mkoa wa Manyara unatarajia kuzindua zoezi la utoaji Huduma za kliniki maalamu za Madaktari Bingwa wa Ndani ya Mkoa Wa Manyara
Na Mzidalfa Zaid
Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema mkoa wa Manyara umeanzisha kliniki ya kwanza ya madaktari bingwa wanaotoka ndani ya mkoa wa Manyara ambao watawahudumia wananchi Kwa gharama za kawaida zinazotumika katika hospital za serikali.
Amesema hayo Leo wakati akiongea na waandish wa habari ofisini kwake , amesema clinic hiyo itazinduliwa November 19 mwaka huu katika wilaya ya Simanjiro na baada ya hapo wilaya zote za mkoa wa Manyara zitanufaika na zoezi Hilo Kwa awamu tofauti.
Amesema mkoa wa Manyara utakuwa mkoa wa kwanza hapa Nchini Kwa kutumia madaktari bingwa wa ndani ya mkoa na huduma hizo zitatolewa kila halmashauri za mkoa wa Manyara kwa miezi tofauti.
Aidha, Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa Manyara Andrew Method, amesema mkoa wa Manyara unaendelea Kupambana na magonjwa mbali mbali yanayojitokeza na lengo la kliniki hiyo ni Kwa ajili ya kuwasaidia wananchi Kwa kuepuka changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.