Wafanyabiashara Manyara watakiwa kuhakiki bidhaa zao TBS
29 October 2024, 7:33 pm
Wafanyabiashara ambao ni wazalishaji wa bidhaa mkoani Manyara wametakiwa kuhakikisha wanakuwa na leseni ya TBS kabla ya kusambaza bidhaa hizo kwa watumiaji ili zihakikiwe ubora.
Na Mzidalfa Zaid
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya kaskazini limewataka wananchi mkoani Manyara ambao ni wazalishaji wa bidhaa kuhakikisha wanakuwa na leseni ya TBS kabla ya kusambaza bidhaa hizo kwa watumiaji ili zihakikiwe ubora.
Wito huo umetolewa leo na afisa masoko mwandamizi kutoka Shirika la Viwango Tanzania TBS kanda ya kaskazini Debora Costantine wakati akiongea na Fm Manyara, amesema TBS imeshiriki kwenye maonesho ya Manyara Tanzanite Trade Fair na imetoa elimu kwa wananchi wengi ambao walihitaji kufahamu kazi kubwa zinazofanywa na TBS.
Amewataka wajasiriamali kufika kwenye banda la TBS lililko katika maeonesho hayo ili kupata elimu kwakuwa leseni zinatolewa bure baada ya serikali kutenga bajeti kwa ajili ya kuwainua wajasiriamali.