FM Manyara

TIRA yawahimiza wananchi kukata bima kujikinga na majanga 

24 October 2024, 6:45 pm

picha ya Meneja wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima  Tanzania Kanda ya kati Frank Fred Shangali

Mamalaka ya usimamizi wa Bima Tanzania(TIRA)kanda ya kati, imewataka wananchi kukata bima kujikinga na majanga ili iwasaidie wanapokutana na majanga ya dharura.

Na Mzidalfa Zaid

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kutembelea banda la Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA lililopo katika maonesho ya Manyara Tanazanite Trade Feir ili wapate elimu  ya umuhimu wa kuwa na bima.

Hayo yamesemwa  leo October 24 2024 na Meneja wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima  Tanzania Kanda ya kati Frank Fred Shangali alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliotembelea banda la TIRA na kujionea namna Taasisi hiyo inavyofanya kazi ikiwemo kutoa elimu.

 Amesema mtu anapokuwa na Bima ni rahisi kusaidika anapokutana na changamoto za dharura ikiwemo ajali ya moto, ajali za barabarani, mafuriko n.k. jambo ambalo linampunguzia maumivu ya kukabiliana na majanga.

sauti ya Meneja wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima  Tanzania Kanda ya kati Frank Fred Shangali

Aidha amewataka wamiliki wa vyombo vya moto yakiwemo mabasi ya kusafirisha abiria kuvikatia bima vyombo vyao ili kuondokana na dhamana ya kulipa fidia kwa mtu yeyote atakayepata majanga kwenye chombo chake.