FM Manyara

Kigahe awataka wanyabiashara kuwa na nembo zinazo watambulisha

24 October 2024, 1:42 pm

Naibu waziri  wa viwanda na biashara Exaud Kigahe amefungua rasmi leo maonyesho ya wanyabiashara Tanzanate Manyara Trade Fear katika viwanja vya stendi ya zamani wilayani Babati mkoani Manyara nakuwataka wafanyabiashara  kuwa na nembo zinazo watambilisha

Na Angel Munuo

Maonyesho ya wanyabiashara Tanzanate Manyara Trade Fear yafunguliwa rasmi leo katika viwanja vya stendi ya zamani wilayani Babati mkoani Manyara na Naibu waziri wa viwanda na biashara Exaud Kigahe ambapo amewataka wafanyabiashara nembo zinazo watambilisha

Wafanya biashara wadogo na wakubwa mkoani Manyara wametakiwa kurasimisha biashara  zao katika mamlaka husika ili wapate nafasi ya kufanya biashara zao ndani na njee ya nchi.

Naibu waziri wa viwanda na biashara Exaud Kigahe ameyasema hayo leo octeber 23 2024 alipomuwakilisha waziri wa viwanda na biashara Sulemani Jafo katika ufunguzi wa maonyesho ya Tanzanate Manyara Trade Fear yanayofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani wilayani Babati mkoani Manyara.

sauti ya Naibu waziri wa viwanda na biashara Exaud Kigahe

Aidha,naibu waziri Kigahe amewataka wajasiriamali nchini kuwa na nembo zinazo watambilisha na kwenda sambamba na kaulimbia ya maenyesho ya 3 ya Manyara Trade Fear isemayo Manyara kwa ustawi wa biashara na uwekezajii.

 kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda ambaye amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga ameipongeza taasisi ya TCCIA Manyara kwa kuandaa maonyesho hayo yenye lengo ya kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara  kwa ajili ya kutangaza biashara zao ikiwa nipamoja na kutangaza utalii wa ndani.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda

Nae  meneja wa kampuni ya uzalishaji vinywaji shangamshi mati super brand ltd Gwandumi Mpoma amesema kampuni ya Mati imekuwa karibu na chemba ya wafanyabiashara kwa kudhamini maonesho na lengo kuu likiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha uwekezaji wa viwanda na biashara pamoja na sekta nyingine.