Wafugaji Simanjiro waaswa kupeleka mabinti shule
7 October 2024, 9:15 pm
Wadau wa elimu kutoka shirika la Kinnapa, wafugaji kutoka wilayani humo wamesema wame elimika kutokana na elimu waliyoipata mara kwa mara na wameamua kuwapeleka watoto wa kike shule na hasa waliopata ujauzito wakiwa na umri mdogo
Na Diana Dionis
Jamii ya wafugaji wilayani Simanjiro mkoani Manyara imetakiwa kuwarejesha wananafunzi walioacha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata mimba za utotoni
Wakizungumza na waandishi wa habari katika kikao kazi cha wadau wa elimu kutoka shirika la kinnapa, wafugaji kutoka wilayani humo wamesema wame elimika kutokana na elimu waliyoipata mara kwa mara na wameamua kuwapeleka watoto wa kike shule na hasa waliopata ujauzito wakiwa na umri mdogo.
Kwa upande wao wadau wa elimu kutoka shirika la kinnapa Paulina Ngurumwa na Onike Laizer wamesema wamepata mafanikio makubwa baada ya kumrejesha mtoto wa kike shule hasa walioacha masomo kwa sababu mbalimbali.
Aidha baadhi ya maafisa ustawi kutoka mkoa wa Manyara wamesema wanaendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuwarejesha watoto wa kike shule ambao wamefanyiwa ukatili nakushindwa kuendelea na masomo yao.