FM Manyara

Wakulima Manyara watakiwa kulima kilimo kisasa cha maharage

September 15, 2024, 4:05 pm

Wakulima mkoani Manyara wametakiwa kutumia mbegu bora kwa kununua sehemu ambazo zinaaminika na siyo kununua kimazoea kwa kupanda mbegu ambazo zinanunuliwa sokoni.

Na Mzidalfa Zaid

Katika kuhakikisha zao la maharage linaendelea kumuinua mkulima kiuchumi, wakulima mkoani Manyara wametakiwa kutumia mbegu bora kwa kununua mbegu hizo sehemu ambazo zinaaminika .

Wito huo umetolewa leo na mtafiti wa kilimo kutoka (TARI) Selian mkoani Arusha Julius Mbiu alipokuwa akiongea na FM Manyara, amesema wakulima wanashauriwa kupanda mimea kwa mstari ili mimea ipate hewa wakati wa ukuaji. 

Sauti ya mtafiti wa kilimo kutoka (TARI) Selian mkoani Arusha Julius Mbiu

Kwa upande wake mkurugenzi wa BIVAC Tanzania Beatrice Msafiri amewataka wakulima kuhakikisha wanatunza vizuri maharage wanapoyavuna ili wapate soko la uhakika kwa kuwa zao hilo lina uhitaji mkubwa.

Aidha, amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa wakulima namna ya kuhifadhi maharage kwa njia bora ambayo inaongeza thamani kwa zao hilo na wamekuwa wakiwasaidia wakulima kuwapatia soko la uhakika.

Sauti ya mkurugenzi wa BIVAC Tanzania Beatrice Msafiri